Yeremia 6:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Enyi watu wa Benyamini,ondokeni Yerusalemu mkimbilie usalama!Pigeni tarumbeta mjini Tekoa;onesheni ishara huko Beth-hakeremu,maana maafa na maangamizi makubwayanakuja kutoka upande wa kaskazini.

2. Mji wa Siyoni ni mzuri na mwororo,lakini utaangamizwa.

3. Watu wataujia kama wachungaji na makundi yao,watapiga hema zao kuuzunguka kila mmoja sehemu yake,wapate kuyaongoza makundi yao.

4. Watasema: “Jitayarisheni kuushambulia Siyoni.Haya! Tuanze kushambulia adhuhuri!Bahati mbaya; jua linatua!Kivuli cha jioni kinarefuka.

5. Basi, tutaushambulia usiku;tutayaharibu majumba yake ya kifalme.”

6. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema:“Kateni miti yake,rundikeni udongo kuuzingira Yerusalemu.Mji huu ni lazima uadhibiwe,maana hamna lolote ndani yake ila dhuluma.

7. Kama kisima kinavyohifadhi maji yake yakabaki safi,ndivyo Yerusalemu unavyohifadhi uovu wako.Ukatili na uharibifu vyasikika ndani yake,magonjwa na majeraha yake nayaona daima.

8. Hilo na liwe onyo kwako ee Yerusalemu,la sivyo nitakutupa kabisa kwa chuki;nikakufanya uwe jangwa,mahali pasipokaliwa na mtu.”

9. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi:“Kusanyeni watu wote wa Israeli waliobakikama watu wakusanyavyo zabibu zote;kama afanyavyo mchumazabibu,pitisheni tena mikono yenu katika matawi yake.”

10. Nitaongea na nani nipate kumwonya,ili wapate kunisikia?Tazama, masikio yao yameziba,hawawezi kusikia ujumbe wako.Kwao neno lako, ee Mwenyezi-Mungu,limekuwa jambo la dhihaka,hawalifurahii hata kidogo.

11. Nimejaa hasira ya Mwenyezi-Mungu dhidi yao.Nashindwa kuizuia ndani yangu.Mwenyezi-Mungu akaniambia:“Imwage hasira barabarani juu ya watotona pia juu ya makundi ya vijana;wote, mume na mke watachukuliwa,kadhalika na wazee na wakongwe.

12. Nyumba zao zitapewa watu wengine,kadhalika na mashamba yao na wake zao;maana nitaunyosha mkono wangu,kuwaadhibu wakazi wa nchi hii.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Yeremia 6