3. la tatu lilikokotwa na farasi weupe, na la nne lilikokotwa na farasi wa kijivujivu.
4. Basi, nikamwuliza yule malaika aliyeongea nami, “Bwana, magari haya ya farasi yanamaanisha nini?”
5. Malaika akanijibu, “Magari haya ni pepo kutoka pande nne za mbingu. Yalikuwa mbele ya Mwenyezi-Mungu wa dunia nzima, na sasa yanaondoka.
6. Lile gari linalokokotwa na farasi weusi linakwenda kaskazini, lile linalokokotwa na farasi weupe linakwenda magharibi, na lile linalokokotwa na farasi wa kijivujivu linakwenda kusini.”
7. Farasi hao walipotokea walikuwa na hamu sana ya kwenda kuikagua dunia. Naye malaika akawaambia, “Haya! Nendeni mkaikague dunia.” Basi, wakaenda na kuikagua dunia.
8. Kisha yule malaika aliyeongea nami akaniambia kwa sauti, “Tazama! Wale farasi waliokwenda nchi ya kaskazini wameituliza ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu.”
9. Neno la Mwenyezi-Mungu likanijia:
10. “Pokea zawadi za watu walio uhamishoni zilizoletwa na Heldai, Tobia na Yedaya. Nenda leo hii nyumbani kwa Yosia, mwana wa Sefania ambamo watu hao wamekwenda baada ya kuwasili kutoka Babuloni.
11. Utachukua fedha na dhahabu hiyo, utengeneze taji ambalo utamvika kuhani mkuu Yoshua, mwana wa Yehosadaki,
12. na kumwambia kuwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: ‘Hapa pana mtu aitwaye Tawi. Yeye atastawi hapo alipo na kulijenga hekalu langu mimi Mwenyezi-Mungu.