5. Basi, tutaushambulia usiku;tutayaharibu majumba yake ya kifalme.”
6. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema:“Kateni miti yake,rundikeni udongo kuuzingira Yerusalemu.Mji huu ni lazima uadhibiwe,maana hamna lolote ndani yake ila dhuluma.
7. Kama kisima kinavyohifadhi maji yake yakabaki safi,ndivyo Yerusalemu unavyohifadhi uovu wako.Ukatili na uharibifu vyasikika ndani yake,magonjwa na majeraha yake nayaona daima.
8. Hilo na liwe onyo kwako ee Yerusalemu,la sivyo nitakutupa kabisa kwa chuki;nikakufanya uwe jangwa,mahali pasipokaliwa na mtu.”
9. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi:“Kusanyeni watu wote wa Israeli waliobakikama watu wakusanyavyo zabibu zote;kama afanyavyo mchumazabibu,pitisheni tena mikono yenu katika matawi yake.”
10. Nitaongea na nani nipate kumwonya,ili wapate kunisikia?Tazama, masikio yao yameziba,hawawezi kusikia ujumbe wako.Kwao neno lako, ee Mwenyezi-Mungu,limekuwa jambo la dhihaka,hawalifurahii hata kidogo.
11. Nimejaa hasira ya Mwenyezi-Mungu dhidi yao.Nashindwa kuizuia ndani yangu.Mwenyezi-Mungu akaniambia:“Imwage hasira barabarani juu ya watotona pia juu ya makundi ya vijana;wote, mume na mke watachukuliwa,kadhalika na wazee na wakongwe.