10. Maana, nchi imejaa wazinzi;kwa sababu ya laana, nchi inaomboleza,na malisho ya nyanda zake yamekauka.Mienendo ya watu ni miovu,nguvu zao zinatumika isivyo halali.
11. Mwenyezi-Mungu asema:“Manabii na makuhani, wote hawamchi Mungu,uovu wao nimeuona hata nyumbani mwangu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
12. Kwa hiyo njia zao zitakuwa vichochoro vya utelezi gizaniambamo watasukumwa na kuanguka;maana, nitawaletea maafa,ufikapo mwaka wa kuwaadhibu,Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
13. “Miongoni mwa manabii wa Samaria,nimeona jambo la kuchukiza sana:Walitabiri kwa jina la Baaliwakawapotosha watu wangu Waisraeli.
14. Lakini miongoni mwa manabii wa Yerusalemu,nimeona kinyaa cha kutisha zaidi:Wanafanya uzinzi na kusema uongo;wanawaunga mkono wanaotenda maovuhata pasiwe na mtu anayeachana na uovu.Kwangu wote wamekuwa kama watu wa Sodoma;wakazi wake wamekuwa wabaya kama watu wa Gomora.
15. “Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema hivi juu ya manabii wa Yerusalemu:Nitawalisha uchungu,na kuwapa maji yenye sumu wanywe.Maana, kutoka kwa manabii wa Yerusalemukutomcha Mungu kumeenea kila mahali nchini.”
16. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Msisikilize maneno ya manabii wanaowatabiria; wanawapeni matumaini ya uongo. Wanayowaambia ni maono yao wenyewe, wala hayakutoka kwangu mimi Mwenyezi-Mungu.
17. Wao hawakomi kuwaambia wale wanaodharau neno langu mimi Mwenyezi-Mungu: ‘Mambo yatawaendea vema.’ Na kumwambia kila mtu afuataye kwa ukaidi fikira zake; ‘Hakuna baya lolote litakalokupata!’”