1. Ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni mwadilifu,ingawa nakulalamikia.Lakini ningependa kutoa hoja zangu mbele yako:Kwa nini waovu hufanikiwa katika mambo yao?Mbona wote wenye hila hustawi?
2. Unawaotesha nao wanaota;wanakua na kuzaa matunda.Wanakutaja kwa maneno yao,lakini mioyo yao iko mbali nawe.
3. Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu wanijua;wayathibiti maelekeo yangu kwako.Uwaokote hao kama kondoo wa kuchinjwa,watenge kwa ajili ya wakati wa kuuawa.
4. Mpaka lini nchi itaomboleza kwa ukame,na nyasi za mashamba yote kunyauka?Wanyama na ndege wanakufa kwa uovu wa wakazi wake;wanasema: “Mungu hataona mwisho wetu.”
5. Mwenyezi-Mungu asema,“Ikiwa umeshindana na waendao kwa miguu ukachoka,utawezaje kushindana na farasi?Kama unaanguka katika nchi isiyo na vizuizi,utafanyaje katika msitu wa Yordani?
6. Hata ndugu zako, jamaa yako mwenyewe,nao pia wamekutendea mambo ya hila;wanakukemea waziwazi.Usiwaamini hata kidogo,japo wanakuambia maneno mazuri.”
7. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nimeiacha nyumba yangu;nimeitupa mali yangu mimi mwenyewe.Israeli, mpenzi wangu wa moyo,nimemtia mikononi mwa maadui zake.