Wimbo Ulio Bora 4:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Hakika u mzuri ewe mpenzi wangu,hakika u mzuri!Macho yako ni kama ya huanyuma ya shela lako,nywele zako ni kama kundi la mbuziwashukao katika milima ya Gileadi.

2. Meno yako ni kama kondoo majike waliokatwa manyoyawanaoteremka baada ya kuogeshwa.Kila mmoja amezaa mapacha,na hakuna yeyote aliyefiwa.

3. Midomo yako ni kama utepe mwekundu,kinywa chako chavutia kweli.Nyuma ya shela lako,mashavu yako ni kama nusu mbili za komamanga.

4. Shingo yako ni kama mnara wa Daudi,uliojengwa ili kuhifadhia silaha,ambako zimetundikwa ngao elfu mojazote zikiwa za mashujaa.

5. Matiti yako ni kama paa mapacha,ambao huchungwa penye yungiyungi.

6. Nitakaa kwenye mlima wa manemane,na kwenye kilima cha ubani,hadi hapo kutakapopambazuka,na giza kutoweka.

Wimbo Ulio Bora 4