Mika 3:4-9 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Wakati unakuja ambapo mtamlilia Mwenyezi-Mungu,lakini yeye hatawajibu.Atauficha uso wake wakati huo,kwa sababu mmetenda mambo maovu.

5. Mwenyezi-Mungu asema hivikuhusu manabii wanaowapotosha watu wake;manabii ambao hutabiri amani wakipewa kitu,lakini huwatishia watu kwa vita wasipopewa kitu:

6. “Kwenu manabii kutakuwa usiku bila maono,kutakuwa giza kwenu bila ufunuo.Kwenu manabii kutakuchwa,mchana utakuwa giza kwenu.”

7. Mabingwa wa maono watafedheheka,mafundi wa kubashiri wataaibishwa;wote watafunga midomo yao,maana hawatapata jibu lolote kutoka kwa Mungu.

8. Lakini kwa upande wangu,nimejazwa nguvu na roho ya Mwenyezi-Mungu;nimejaliwa kujua haki na kuwa na uwezoniwatangazie wazawa wa Yakobo kosa lao,niwaambie Waisraeli dhambi yao.

9. Sikieni jambo hili enyi viongozi wa wazawa wa Yakobo,sikilizeni, enyi watawala wa Waisraeli:Nyinyi mnachukia mambo ya hakina kupotosha mambo ya adili.

Mika 3