10. Na wawafundishe wazawa wa Yakobo maagizo yako;wawafundishe watu wa Israeli sheria yako.Walawi na wafukize ubani mbele yako,sadaka nzima za kuteketezwa madhabahuni pako.
11. Ee Mwenyezi-Mungu, uzibariki nguvu zao,uzikubali kazi za mikono yao;uzivunjilie mbali nguvu za maadui zao,nguvu za wanaowachukia hata wasiinuke tena.”
12. Juu ya kabila la Benyamini alisema:“Hili ni kabila alipendalo Mwenyezi-Mungu,nalo hukaa salama karibu naye.Yeye hulilinda mchana kutwa,na kukaa kati ya milima yake.”
13. Juu ya kabila la Yosefu alisema:“Mwenyezi-Mungu na aibariki nchi yake,kwa baraka nzuri kabisa kutoka juu,
14. ibarikiwe kwa matunda bora yalioiva kwa jua,kwa matunda ya kila mwezi;
15. kwa mazao bora ya milima ya kale,na mazao tele ya milima ya kale,