4. Watu wa Heshboni na Eleale wanalia,sauti zao zinasikika hadi Yahazi.Hata askari wa Moabu wanalia kwa sauti;mioyo yao inatetemeka.
5. Moyo wangu unasononeka juu ya nchi ya Moabu;wakimbizi wake wanakimbilia Soari,wanakimbia mpaka Eglath-shelishiya.Wanapanda njia ya kwenda Luhithi wakilia,njiani kwenda Horonaimu wanatoa kilio cha maangamizi.
6. Kijito cha Nimrimu kimekauka;nyasi zimekauka, majani mabichi yamenyauka,hakuna chochote kinachoota hapo.
7. Watu wanavuka kijito cha Mierebiwamebeba mali yao yote waliyochuma,na kila walichojiwekea kama akiba.
8. Kilio kimezuka pote nchini Moabu,maombolezo yao yamefika Eglaimu,naam, yamefika mpaka Beer-elimu.
9. Maji ya Diboni yamejaa damu,lakini Mungu ataongeza msiba wa Diboni.Hao wachache watakaobaki haina kukimbia kutoka nchini Moabu,watapelekewa simba wa kuwaua.