1. Kauli ya Mungu dhidi ya nchi ya Moabu.Mji wa Ari nchini Moabu umeangamizwa usiku;mji wa Kiri nchini Moabu umeteketezwa usiku.
2. Watu wa Diboni wamepanda hekaluni, hadi mahali pa juu kuomboleza,watu wa Moabu wanalia kwa ajili ya Nebo na Medeba;vichwa vyote vimenyolewa upara,ndevu zao zote zimekatwa kabisa.
3. Wanapita njiani wamevaa mavazi ya gunia.Kwenye paa za nyumba na viwanja vya mjiwatu wanalia na kukauka kwa machozi.
4. Watu wa Heshboni na Eleale wanalia,sauti zao zinasikika hadi Yahazi.Hata askari wa Moabu wanalia kwa sauti;mioyo yao inatetemeka.
5. Moyo wangu unasononeka juu ya nchi ya Moabu;wakimbizi wake wanakimbilia Soari,wanakimbia mpaka Eglath-shelishiya.Wanapanda njia ya kwenda Luhithi wakilia,njiani kwenda Horonaimu wanatoa kilio cha maangamizi.