Isaya 14:7-12 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Sasa dunia yote ina utulivu na amani,kila mtu anaimba kwa furaha.

8. Misonobari inafurahia kuanguka kwako,nayo mierezi ya Lebanoni pamoja yasema:‘Kwa vile sasa umeangushwa,hakuna mkata miti atakayekuja dhidi yetu!’

9. “Kuzimu nako kumechangamka,ili kukulaki wakati utakapokuja.Kunaiamsha mizimu ije kukusalimuna wote waliokuwa wakuu wa dunia;huwaamsha kutoka viti vyao vya enziwote waliokuwa wafalme wa mataifa.

10. Wote kwa pamoja watakuambia:‘Nawe pia umedhoofika kama sisi!Umekuwa kama sisi wenyewe!

11. Fahari yako imeteremshwa kuzimupamoja na muziki wa vinubi vyako.Chini mabuu ndio kitanda chako,na wadudu ndio blanketi lako!’

12. “Jinsi gani ulivyoporomoshwa toka mbinguni,wewe uliyekuwa nyota angavu ya alfajiri.Jinsi gani ulivyoangushwa chini,wewe uliyeyashinda mataifa!

Isaya 14