4. Sikilizeni kelele milimanikama za kundi kubwa la watu!Sikilizeni kelele za falme,na mataifa yanayokusanyika!Mwenyezi-Mungu wa majeshianalikagua jeshi linalokwenda vitani.
5. Wanakuja kutoka nchi za mbali,wanatoka hata miisho ya dunia:Mwenyezi-Mungu na silaha za hasira yakeanakuja kuiangamiza dunia.
6. Lieni maana siku ya Mwenyezi-Mungu imekaribia;inakuja kama maafa kutoka kwa Mungu Mwenye Nguvu.
7. Kwa hiyo mikono ya kila mtu italegea,kila mtu atakufa moyo.
8. Watu watafadhaika,watashikwa na hofu na maumivu,watakuwa na uchungu kama mama anayejifungua.Watatazamana kwa mashaka,nyuso zao zitawaiva kwa haya.
9. Siku ya Mwenyezi-Mungu inakuja,siku kali, ya ghadhabu na hasira kali.Itaifanya nchi kuwa uharibifu,itawaangamiza wenye dhambi wake.
10. Nyota na vilimia vyake angani hazitaangaza;jua linapochomoza litakuwa giza,na mwezi hautatoa mwanga wake.
11. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nitauadhibu ulimwengu kwa uovu wake,waovu kwa sababu ya makosa yao.Nitakikomesha kiburi cha wenye majivuno,na kuporomosha ubaradhuli wa watu katili.
12. Nitawafanya watu kuwa wachache kuliko dhahabu safi;binadamu watakuwa wachache kuliko dhahabu ya Ofiri.
13. Nitazitetemesha mbingunayo nchi itatikisika katika misingi yakekwa sababu ya ghadhabu yangu Mwenyezi-Mungusiku ile ya hasira yangu kali.
14. “Kama swala anayewindwa,kama kondoo wasio na mchungaji,kila mmoja atajiunga na watu wakekila mtu atakimbilia nchini mwake.
15. Yeyote atakayeonekana atatumbuliwa,atakayekamatwa atauawa kwa upanga.