1. Waisraeli walikuwa kama mzabibu mzuri,mzabibu wenye kuzaa matunda.Kadiri matunda yalivyozidi kuongezeka,ndivyo walivyozidi kujijengea madhabahu.Kadiri nchi yao ilivyozidi kustawi,ndivyo walivyozidi kupamba nguzo zao za ibada.
2. Mioyo yao imejaa udanganyifu.Sasa ni lazima wawajibike kwa hatia yao.Mwenyezi-Mungu atazibomoa madhabahu zaona kuziharibu nguzo zao.
3. Wakati huo watasema:“Hatuna tena mfalme,kwa kuwa hatumchi Mwenyezi-Mungu;lakini, naye mfalme atatufanyia nini?”
4. Wanachosema ni maneno matupu;wanaapa na kufanya mikataba ya bure;haki imekuwa si haki tena,inachipua kama magugu ya sumu shambani.
5. Wakazi wa Samaria watatetemekakwa sababu ya ndama wa huko Betheli.Watu wake watamwombolezea ndama huyo,hata makuhani wanaomwabudu watamlilia;kwani fahari ya ndama huyo imeondolewa.
6. Kinyago hicho kitapelekwa Ashuru,kama ushuru kwa mfalme mkuu.Watu wa Efraimu wataaibishwa,Waisraeli watakionea aibu kinyago chao.