Amosi 4:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Sikilizeni neno hili,enyi wanawake ng'ombe wa Bashanimlioko huko mlimani Samaria;nyinyi mnaowaonea wanyonge,mnaowakandamiza maskini,na kuwaambia waume zenu:“Tuleteeni divai tunywe!”Sikilizeni ujumbe huu:

2. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu Mtakatifu nimeapa:“Tazama, siku zaja,ambapo watu watawakokoteni kwa kulabu,kila mmoja wenu kama samaki kwenye ndoana.

3. Mtaburutwa hadi ukutani palipobomolewa,na kutupwa nje.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.

4. “Enyi Waisraeli,nendeni basi huko Betheli mkaniasi!Nendeni Gilgali mkalimbikize makosa yenu!Toeni sadaka zenu kila asubuhi,na zaka zenu kila siku ya tatu.

5. Toeni tambiko ya shukrani ya mikate iliyochachushwa.Tangazeni popote kwamba mmetoa kwa hiari;kwani ndivyo mnavyopenda kufanya!Mimi Bwana Mungu nimenena.

6. “Mimi niliwanyima chochote cha kutafuna,nikasababisha ukosefu wa chakula popote.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.

7. “Tena niliwanyima mvuamiezi mitatu tu kabla ya mavuno.Niliunyeshea mvua mji mmoja,na mji mwingine nikaunyima.Shamba moja lilipata mvua,na lingine halikupata, likakauka.

8. Watu wa miji miwili, mitatu wakakimbilia mji mwingine,wapate maji, lakini hayakuwatosha.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.

Amosi 4