Amosi 2:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Moabu wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Wamemkosea heshima marehemu mfalme wa Edomukwa kuichoma moto mifupa yakeili kujitengenezea chokaa!

2. Basi, nitaishushia moto nchi ya Moabu,na kuziteketeza kabisa ngome za mji wa Keriothi.Wanajeshi watakapopaza sauti zao na kupiga tarumbeta,watu wa Moabu watakufa katika makelele hayo ya vita.

3. Isitoshe, nitamuua mtawala wa Moabu,pamoja na viongozi wote wa nchi hiyo.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

4. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Yuda wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Wamepuuza sheria zangu,wala hawakufuata amri zangu.Wamepotoshwa na miungu ileile waliyoihudumia wazee wao.

5. Basi, nitaishushia moto nchi ya Yuda,na kuziteketeza kabisa ngome za Yerusalemu.”

6. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Waisraeli wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Wamewauza watu waaminifukwa kuwa hawakuweza kulipa madeni yao;na kuwauza watu fukarawasioweza kulipa deni la kandambili.

7. Huwanyanyasa na kuwakandamiza wanyonge,na maskini huwabagua wasipate haki zao.Mtu na baba yake hulala na mjakazi yuleyule,hivyo hulitia unajisi jina langu takatifu.

8. Popote penye madhabahu,watu hulalia nguo walizotwaa kwa maskinikama dhamana ya madeni yao;na katika nyumba ya Mungu waohunywa divai waliyotwaa kwa wadeni wao.

9. “Hata hivyo, enyi watu wangu,kwa ajili yenu, niliwaangamiza kabisa Waamoriambao walikuwa wakubwa kama mierezi,wenye nguvu kama miti ya mialoni.Naam, niliwaangamiza, matawi na mizizi.

Amosi 2