Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Yuda wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Wamepuuza sheria zangu,wala hawakufuata amri zangu.Wamepotoshwa na miungu ileile waliyoihudumia wazee wao.