Zekaria 9:10-17 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Atatokomeza magari ya vita nchini Efraimu,na farasi wa vita kutoka mjini Yerusalemu;pinde za vita zitavunjiliwa mbali.Naye ataleta amani miongoni mwa mataifa;utawala wake utaenea toka bahari hata bahari,toka mto Eufrate hata miisho ya dunia.

11. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Kwa sababu ya agano langu nanyi,agano lililothibitishwa kwa damu,nitawakomboa wafungwa wenuwalio kama wamefungwa katika shimo tupu.

12. Enyi wafungwa wenye tumaini;rudini kwenye ngome yenu.Sasa mimi ninawatangazieni:Nitawarudishieni mema maradufu.

13. Yuda nitamtumia kama uta wangu;Efraimu nimemfanya mshale wangu.Ee Siyoni! Watu wako nitawatumia kama upangakuwashambulia watu wa Ugiriki;watakuwa kama upanga wa shujaa.”

14. Mwenyezi-Mungu atawatokea watu wake;atafyatua mishale yake kama umeme.Bwana Mwenyezi-Mungu atapiga tarumbeta;atafika pamoja na kimbunga cha kusini.

15. Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawalinda watu wake,nao watawaangamiza maadui zao.Watapiga kelele vitani kama waleviwataimwaga damu ya maadui zao.Itatiririka kama damu ya tambikoiliyomiminwa madhabahuni kutoka bakulini.

16. Wakati huo, Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, atawaokoa,maana wao ni kundi lake;nao watang'aa katika nchi yakekama mawe ya thamani katika taji.

17. Jinsi gani uzuri na urembo wake ulivyo!Wavulana na wasichana watanawirikwa wingi wa nafaka na divai mpya.

Zekaria 9