1. Neno la Mwenyezi-Mungu lililomjia nabii Yeremia kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajaushambulia mji wa Gaza:
2. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Tazama! Maji yanapanda kutoka kaskazini,nayo yatakuwa mto uliofurika;yataifunika nchi nzima na vyote vilivyomo,mji na wakazi na wanaoishi humo.Watu watalia,wakazi wote wa nchi wataomboleza.
3. Watasikia mshindo wa kwato za farasi,kelele za magari ya vita,na vishindo vya magurudumu yao.Kina baba watawasahau watoto wao,mikono yao itakuwa imelegea mno.