Yeremia 25:32-38 Biblia Habari Njema (BHN)

32. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema:“Tazama, maafa yatalikumba taifa moja baada ya lingine,na tufani itazuka kutoka miisho ya dunia.”

33. Siku hiyo, watakaouawa na Mwenyezi-Mungu watatapakaa kutoka upande mmoja wa dunia hadi mwingine. Hawataombolezewa, hawatakusanywa wala kuzikwa; watabaki kuwa mavi juu ya ardhi.

34. Ombolezeni enyi wachungaji;lieni na kugaagaa majivuni enyi wakuu wa kundi;siku za kuchinjwa kwenu na kutawanywa zimefika;mtauawa kama kondoo madume waliochaguliwa.

35. Wachungaji hawatakuwa na pa kukimbilia,wala wakuu wa kundi hawataweza kutoroka.

36. Sikilizeni kilio cha wachungajina mayowe ya wakuu wa kundi!Mwenyezi-Mungu anayaharibu malisho yao,

37. na makundi yaliyokuwa matulivu yameharibiwakwa sababu ya hasira kali ya Mwenyezi-Mungu.

38. Mwenyezi-Mungu amewaacha watu wake,kama vile simba aachavyo pango lake;nchi yao imekuwa jangwa tupu,kwa sababu ya vita vya wadhalimu,na hasira kali ya Mwenyezi-Mungu.

Yeremia 25