Yeremia 23:11-17 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Mwenyezi-Mungu asema:“Manabii na makuhani, wote hawamchi Mungu,uovu wao nimeuona hata nyumbani mwangu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

12. Kwa hiyo njia zao zitakuwa vichochoro vya utelezi gizaniambamo watasukumwa na kuanguka;maana, nitawaletea maafa,ufikapo mwaka wa kuwaadhibu,Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

13. “Miongoni mwa manabii wa Samaria,nimeona jambo la kuchukiza sana:Walitabiri kwa jina la Baaliwakawapotosha watu wangu Waisraeli.

14. Lakini miongoni mwa manabii wa Yerusalemu,nimeona kinyaa cha kutisha zaidi:Wanafanya uzinzi na kusema uongo;wanawaunga mkono wanaotenda maovuhata pasiwe na mtu anayeachana na uovu.Kwangu wote wamekuwa kama watu wa Sodoma;wakazi wake wamekuwa wabaya kama watu wa Gomora.

15. “Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema hivi juu ya manabii wa Yerusalemu:Nitawalisha uchungu,na kuwapa maji yenye sumu wanywe.Maana, kutoka kwa manabii wa Yerusalemukutomcha Mungu kumeenea kila mahali nchini.”

16. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Msisikilize maneno ya manabii wanaowatabiria; wanawapeni matumaini ya uongo. Wanayowaambia ni maono yao wenyewe, wala hayakutoka kwangu mimi Mwenyezi-Mungu.

17. Wao hawakomi kuwaambia wale wanaodharau neno langu mimi Mwenyezi-Mungu: ‘Mambo yatawaendea vema.’ Na kumwambia kila mtu afuataye kwa ukaidi fikira zake; ‘Hakuna baya lolote litakalokupata!’”

Yeremia 23