Yeremia 21:12-14 Biblia Habari Njema (BHN)

12. enyi jamaa ya Daudi! Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Tekelezeni haki tangu asubuhi,na kuwakomboa mikononi mwa wadhalimuwote walionyanganywa mali zao.La sivyo, hasira yangu itachomoza kama moto,itawaka na wala hakuna atakayeweza kuizima,kwa sababu ya matendo yenu maovu.

13. Tazama, mimi sasa napambana nanyi mnaoishi bondeni,mnaokaa kwenye mwamba wa tambarare,nyinyi mnaosema, ‘Nani atathubutu kutushambulia?Nani awezaye kuingia katika makazi yetu?’

14. Nitawaadhibu kadiri ya matendo yenu;mimi Mwenyezi-Mungu nasema.Nitawasha moto katika msitu wenunao utateketeza kila kitu kinachouzunguka.”

Yeremia 21