26. “Kama vile mwizi aonavyo aibu akishikwa,ndivyo Waisraeli watakavyoona aibu;wao wenyewe, wafalme wao, wakuu wao,makuhani wao na manabii wao.
27. Hao huuambia mti: ‘Wewe u baba yangu,’na jiwe: ‘Wewe ndiwe uliyenizaa;’kwa maana wamenipa kisogo,wala hawakunielekezea nyuso zao.Lakini wakati wa shida husema: ‘Inuka utuokoe!’
28. “Lakini iko wapi miungu yako uliyojifanyia?Iinuke basi, kama inaweza kukusaidia,wakati unapokuwa katika shida.Ee Yuda, idadi ya miungu yakoni sawa na idadi ya miji yako!
29. Mbona mnanilalamikia?Nyinyi nyote mmeniasi.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
30. Niliwaadhibu watu wako bila kufanikiwa,wao wenyewe walikataa kukosolewa.Upanga wako uliwamaliza manabii wakokama simba mwenye uchu.
31. Enyi watu! Sikilizeni ninachosema mimi Mwenyezi-Mungu:Je, nimekuwa jangwa kwa Israeliau nchi yenye giza nene?Kwa nini basi watu wangu waseme:‘Sisi tu watu huru;hatutakuja kwako tena!’
32. Kijana msichana aweza kusahau mapambo yakeau bibi arusi mavazi yake?Lakini watu wangu wamenisahaukwa muda wa siku zisizohesabika.
33. Kweli wewe ni bingwa wa kutafuta wapenzi!Hata wanawake wabaya huwafundisha njia zako.