21. Lakini mimi nilikupanda kama mzabibu mteule,mzabibu wenye afya na wa mbegu safi;mbona basi umeharibika,ukageuka kuwa mzabibu mwitu?
22. Hata ukijiosha kwa magadi,na kutumia sabuni nyingi,madoa ya uovu wako bado yatabaki mbele yangu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
23. “Unawezaje kusema, ‘Mimi si najisi;sijawafuata Mabaali?’Tazama ulivyotenda dhambi kule bondeni;angalia ulivyofanya huko!Wewe ni kama mtamba wa ngamia,akimbiaye huko na huko;
24. kama pundamwitu aliyezoea jangwani.Katika tamaa yake hunusanusa upepo;nani awezaye kuizuia hamu yake?Amtakaye hana haja ya kujisumbua;wakati wake ufikapo watampata tu.
25. Israeli, usiichakaze miguu yakowala usilikaushe koo lako.Lakini wewe wasema: ‘Hakuna tumaini lolote.Nimeipenda miungu ya kigeni,hiyo ndiyo nitakayoifuata.’