1. Mwangamizi amekuja kukushambulia ee Ninewi.Chunga ngome zako!Weka ulinzi barabarani!Jiweke tayari!Kusanya nguvu zako zote!
2. Mwenyezi-Mungu anamrudishia Yakobo fahari yake,naam, anawapa tena Waisraeli fahari yao,ingawa wavamizi hawakuwaachia kitu,hata matawi yao ya mizabibu waliyakata.
3. Ngao za mashujaa wake ni nyekundu,askari wake wamevaa mavazi mekundu sana.Magari yao ya farasi yanamulika kama miali ya moto,yamepangwa tayari kushambulia;farasi hawatulii kwa uchu wa kushambulia.
4. Magari ya farasi yanatimua mbio barabarani,yanakwenda huko na huko uwanjani.Yanamulika kama miali ya moto!Yanakwenda kasi kama umeme.
5. Sasa anawaita maofisa wake,nao wanajikwaa wanapomwendea;wanakwenda ukutani himahimakutayarisha kizuizi.
6. Vizuizi vya mito vimefunguliwa,ikulu imejaa hofu.
7. Mji uko wazi kabisa,watu wamechukuliwa mateka.Wanawake wake wanaomboleza,wanalia kama njiwa,na kujipigapiga vifuani.
8. Ninewi ni kama bwawa lililobomoka,watu wake wanaukimbia ovyo.“Simameni! Simameni!” Sauti inaita,lakini hakuna anayerudi nyuma.
9. “Chukueni nyara za fedha,chukueni nyara za dhahabu!Hazina yake haina mwisho!Kuna wingi wa kila kitu cha thamani!”