Maombolezo 2:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu, kwa hasira yake,amewaweka watu wa Siyoni gizani.Fahari ya Israeli ameibwaga chini.Siku ya hasira yakealilitupilia mbali hata hekalu lake.

2. Mwenyezi-Mungu ameharibu bila hurumamakazi yote ya wazawa wa Yakobo.Kwa ghadhabu yake amezibomoa ngome za watu wa Yuda.Ufalme wao na watawala wakeameuporomosha chini kwa aibu.

3. Nguvu yote ya Israeli ameivunja kwa hasira.Hakunyosha mkono kuwasaidiawalipokutana na adui;amewawakia watu wa Yakobo kama moto,akateketeza kila kitu.

4. Amevuta upinde wake kama adui,na kuuweka mkono wake wa kulia tayari,amewaua wote tuliowaonea faharikatika maskani yetu watu wa Siyoni.Ametumiminia hasira yake kama moto.

5. Mwenyezi-Mungu amekuwa kama adui,ameangamiza watu wa Israeli;majumba yake yote ameyaharibu,ngome zake amezibomoa.Amewazidishia watu wa Yudamatanga na maombolezo.

6. Hekalu lake amelibomoa kama kitalu bustanini,maskani yake ameiharibu.Amefutilia mbali sikukuu na Sabato huko Siyoni,kwa hasira yake kuu amewakataa mfalme na makuhani.

Maombolezo 2