Kutoka 15:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Hapo, Mose pamoja na Waisraeli wakamwimbia Mwenyezi-Mungu wimbo huu,“Nitamwimbia Mwenyezi-Mungu kwani ameshinda kwa fahari,farasi na mpandafarasi wake amewatosa baharini.

2. Mwenyezi-Mungu hunijalia nguvu na uwezo,yeye mwenyewe ndiye anayeniokoa.Yeye ni Mungu wangu nami nitamsifu,ni Mungu wa baba yangu nami nitamtukuza.

3. Mwenyezi-Mungu ni shujaa vitani;Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake.

4. “Magari na majeshi ya Farao ameyatumbukiza baharini,maofisa wake wateule wamezama katika bahari ya Shamu.

5. Vilindi vya maji vimewafunika,wameporomoka baharini kama jiwe.

Kutoka 15