38. Iko wapi hiyo miungu iliyokula matoleo yenuna kunywa divai na tambiko zenu za kinywaji?Basi na iinuke, iwasaidieni;acheni hiyo iwe kinga yenu sasa!
39. Oneni kuwa mimi ndimi Munguna wala hakuna mwingine ila mimi.Mimi huua na kuweka hai;hujeruhi na kuponya,na hakuna awezaye kumwokoa yeyote mikononi mwangu.
40. Nanyosha mkono wangu mbinguni,na kuapa, kwa uhai wangu wa milele,
41. kama mkiuona upanga wangu umeremetao,na kunyosha mkono kutoa hukumu,nitawalipiza kisasi maadui zangu,nitawaadhibu wale wanaonichukia.
42. Mishale yangu nitailevya kwa damu,upanga wangu utashiba nyama,utalowa damu ya majeruhi na matekana adui wenye nywele ndefu.
43. “Enyi mataifa washangilieni watu wake,maana yeye hulipiza kisasi damu ya watumishi wake,huwalipiza kisasi wapinzani wake,na kuitakasa nchi ya watu wake.”
44. Mose alikuja mbele ya Yoshua, mwana wa Nuni, wakakariri maneno ya wimbo huu, ili Waisraeli wote wausikie.
45. Mose alipomaliza kuwaambia watu wa Israeli maneno haya yote,
46. aliwaambia, “Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo ninawapeni leo. Lazima muwaamuru watoto wenu ili wafuate kwa uaminifu maneno yote ya sheria hii.
47. Maana sheria hii si maneno matupu bali ni uhai wenu; kwa sheria hii mtaishi maisha marefu katika nchi mnayokwenda kuimiliki, ngambo ya mto Yordani.”
48. Siku hiyohiyo, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose,