Kumbukumbu La Sheria 14:15-25 Biblia Habari Njema (BHN)

15. mbuni, kirukanjia, dudumizi, kipanga kwa aina zake,

16. bundi, mumbi, bundi mkubwa,

17. mwari, nderi, mnandi,

18. membe, koikoi kwa aina zake, hudihudi na popo.

19. Na wadudu wote wenye mabawa ni najisi kwenu; msiwale.

20. Mnaweza kula viumbe vyote vyenye mabawa vilivyo safi.

21. Msile nyamafu yoyote; mnaweza kumpa mgeni anayeishi katika miji yenu, ale, au mnaweza kumwuzia mtu wa taifa lingine, kwa sababu nyinyi ni watakatifu na Mwenyezi-Mungu ni Mungu wenu. Msimchemshe mwanambuzi katika maziwa ya mama yake.

22. “Toeni sehemu moja ya kumi ya mazao yenu yote ya shambani kila mwaka.

23. Halafu nendeni mahali ambapo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu amepachagua kuweka jina lake, na mkiwa mbele yake mtaila zaka ya nafaka yenu, ya divai yenu na ya mafuta, na ya wazaliwa wa kwanza wa ng'ombe na kondoo wenu; fanyeni hivi ili mjifunze kumcha Mwenyezi-Mungu Mungu wenu daima.

24. Ikiwa safari ni ndefu kwa kuwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amechagua mahali pa kuweka jina lake ambapo ni mbali mno na nyumbani, nanyi hamwezi kubeba zaka za mazao yenu ambayo Mwenyezi-Mungu amewajalia kupata, basi, fanyeni hivi:

25. “Uzeni mazao yenu na kuchukua fedha hiyo mpaka mahali Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alipopachagua,

Kumbukumbu La Sheria 14