Isaya 58:3-7 Biblia Habari Njema (BHN)

3. “Nyinyi mnaniuliza:‘Mbona tunafunga lakini wewe huoni?Mbona tunajinyenyekesha, lakini wewe hujali?’“Ukweli ni kwamba wakati mnapofunga,mnatafuta tu furaha yenu wenyewe,na kuwakandamiza wafanyakazi wenu!

4. Mnafunga, na kugombana na kupigana ngumi.Mkifunga namna hiyomaombi yenu hayatafika kwangu juu.

5. Mfungapo, nyinyi mnajitaabisha;mnaviinamisha vichwa vyenu kama unyasi,na kulalia nguo za magunia na majivu.Je, huo ndio mnaouita mfungo?Je, hiyo ni siku inayokubaliwa nami?

6. “La! Mfungo ninaotaka mimi ni huu:Kuwafungulia waliofungwa bila haki,kuziondoa kamba za utumwa,kuwaachia huru wanaokandamizwa,na kuvunjilia mbali udhalimu wote!

7. Mfungo wa kweli ni kuwagawia wenye njaa chakula chako,kuwakaribisha nyumbani kwako maskini wasio na makao,kuwavalisha wasio na nguo,bila kusahau kuwasaidia jamaa zenu.

Isaya 58