Kwa hiyo aliwamwagia hasira yake kali,akawaacha wakumbane na vita vikali.Hasira yake iliwawakia kila upande,lakini wao hawakuelewa chochote;iliwachoma, lakini hawakutilia jambo hilo maanani.