Isaya 42:10-14 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Mwimbieni Mwenyezi-Mungu wimbo mpya!Dunia yote iimbe sifa zake:Bahari na vyote vilivyomo,nchi za mbali na wakazi wake;

11. jangwa na miji yake yote ipaaze sauti,vijiji vya wakazi wa Kedari vimsifu,wakazi wa Sela waimbe kwa shangwe;wapaaze sauti kutoka mlimani juu.

12. Wote wakaao nchi za mbali,na wamtukuze na kumsifu Mwenyezi-Mungu.

13. Mwenyezi-Mungu ajitokeza kama shujaa;kama askari vitani ajikakamua kupigana.Anapaza sauti kubwa ya vita,na kujionesha mwenye nguvu dhidi ya maadui zake.

14. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Kwa muda mrefu sasa nimenyamaza,nimekaa kimya na kujizuia;lakini sasa nitalia kama mama anayejifungua,anayetweta pamoja na kuhema.

Isaya 42