Hosea 14:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Watarudi na kuishi chini ya ulinzi wangu,watastawi kama bustani nzuri.Watachanua kama mzabibu,harufu yao nzuri kama ya divai ya Lebanoni.

8. Enyi watu wa Efraimu,mna haja gani tena na sanamu?Mimi ndiye ninayesikiliza sala zenu,mimi ndiye ninayewatunzeni.Mimi nitawapa kivuli kama mberoshi,kutoka kwangu mtapata matunda yenu.

9. Yeyote aliye na hekima ayaelewe mambo haya,mtu aliye na busara ayatambue.Maana njia za Mwenyezi-Mungu ni nyofu;watu wanyofu huzifuata,lakini wakosefu hujikwaa humo.”

Hosea 14