Hosea 10:4-9 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Wanachosema ni maneno matupu;wanaapa na kufanya mikataba ya bure;haki imekuwa si haki tena,inachipua kama magugu ya sumu shambani.

5. Wakazi wa Samaria watatetemekakwa sababu ya ndama wa huko Betheli.Watu wake watamwombolezea ndama huyo,hata makuhani wanaomwabudu watamlilia;kwani fahari ya ndama huyo imeondolewa.

6. Kinyago hicho kitapelekwa Ashuru,kama ushuru kwa mfalme mkuu.Watu wa Efraimu wataaibishwa,Waisraeli watakionea aibu kinyago chao.

7. Mfalme wa Samaria atachukuliwa,kama kipande cha mti juu ya maji.

8. Mahali pa kuabudia vilimani pa Aweni,dhambi ya Waisraeli, pataharibiwa.Miiba na magugu vitamea katika madhabahu zao.Nao wataiambia milima, “Tufunikeni”na vilima, “Tuangukieni!”

9. Enyi Waisraeli,nyinyi mmetenda dhambi tangu kule Gibea,na bado mnaendelea.Hakika vita vitawaangamiza hukohuko Gibea.

Hosea 10