Amosi 9:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Nilimwona Mwenyezi-Mungu amesimama kando ya madhabahu, naye akaniamuru:“Zipige hizo nguzo za hekalumpaka misingi yake itikisike.Zivunje hizo nguzo ziwaangukie watu vichwani.Wale watakaosalia nitawaua kwa upanga;hakuna hata mmoja wao atakayenusurika,naam, hakuna atakayetoroka.

2. Wajapojichimbia njia ya kwenda kuzimu,huko nitawachukua kwa mkono wangu;wajapopanda mbinguni,nitawaporomosha chini.

3. Wajapojificha juu ya mlima Karmeli,huko nitawasaka na kuwachukua;wajapojificha mbali nami vilindini mwa bahari,humo nitaliamuru joka la baharini liwaume.

4. Wajapochukuliwa mateka na adui zao,huko nitatoa amri wauawe kwa upanga.Nitawachunga kwa makini sananiwatendee mabaya na si mema.”

Amosi 9