5. Lakini msinitafute huko Betheliwala msiende Gilgaliwala msivuke kwenda Beer-sheba.Maana wakazi wa Gilgali,hakika watachukuliwa uhamishoni,na Betheli utaangamizwa!”
6. Mtafuteni Mwenyezi-Mungu, nanyi mtaishi!La sivyo, atawalipukia wazawa wa Yosefu kama moto;moto utawateketeza wakazi wa Bethelina hakuna mtu atakayeweza kuuzima.
7. Tahadhari enyi mnaogeuza haki kuwa uchungu,na kuuona uadilifu kuwa kama takataka!
8. Huyo aliyezifanya Kilimia na sayari Orioni,ambaye huligeuza giza nene kuwa mchana,na mchana kuwa usiku;yeye ambaye ayaitaye pamoja maji ya baharina kuyamwaga juu ya nchi kavu,Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake.
9. Yeye ndiye anayewaangamiza wenye nguvu,na kuziharibu ngome zao.
10. Nyinyi huwachukia watetezi wa hakina wenye kusema ukweli mahakamani.
11. Nyinyi mnawakandamiza fukarana kuwatoza kodi ya ngano kupita kiasi.Mnajijengea nyumba za mawe ya kuchonga,lakini nyinyi hamtaishi humo;mnalima bustani nzuri za mizabibu,lakini hamtakunywa divai yake.
12. Maana mimi najua wingi wa makosa yenuna ukubwa wa dhambi zenu;nyinyi mnawatesa watu wema,mnapokea rushwana kuzuia fukara wasipate haki mahakamani.
13. Basi, kutakuwa na wakati mbayaambao hata mwenye busara atanyamaza.
14. Tafuteni kutenda mema na si mabaya,ili nyinyi mpate kuishinaye Mwenyezi-Mungu wa majeshiawe pamoja nanyi kama mnavyosema.
15. Chukieni uovu, pendeni wema,na kudumisha haki mahakamani.Yamkini Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawafadhili watu wa Yosefu waliobaki.