8. Simba akinguruma,ni nani asiyeogopa?Bwana Mwenyezi-Mungu akinena,ni nani atakataa kuutangaza ujumbe wake?
9. Tangazeni katika ikulu za Ashdodi,na katika ikulu za nchi ya Misri:“Kusanyikeni kwenye milimainayoizunguka nchi ya Samaria,mkajionee msukosuko mkubwana dhuluma zinazofanyika humo.”
10. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu hawa wameyajaza majumba yaovitu vya wizi na unyang'anyi.Hawajui kabisa kutenda yaliyo sawa!
11. Kwa hiyo, adui ataizingira nchi yao,atapaharibu mahali pao pa kujihami,na kuziteka nyara ikulu zao.”