Amosi 3:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Enyi Waisraeli, sikilizeni neno Mwenyezi-Mungu alilosema dhidi yenu, enyi taifa zima alilolitoa nchini Misri:

2. “Kati ya mataifa yote ulimwenguni,ni nyinyi tu niliowachagua.Kwa hiyo nitawaadhibu nyinyi,kwa sababu ya uovu wenu wote.”

3. Je, watu wawili huanza safari pamoja,bila ya kufanya mpango pamoja kwanza?

4. Je, simba hunguruma porinikama hajapata mawindo?Je, mwanasimba hunguruma pangoni mwakekama hajakamata kitu?

5. Je, mtego bila chamboutamnasa ndege?Je, mtego hufyatukabila kuguswa na kitu?

6. Je, baragumu ya vita hulia mjinibila kutia watu hofu?Je, mji hupatwa na jangaasilolileta Mungu?

7. Hakika, Bwana Mwenyezi-Mungu hafanyi kitubila kuwafunulia watumishi wake manabii nia yake.

8. Simba akinguruma,ni nani asiyeogopa?Bwana Mwenyezi-Mungu akinena,ni nani atakataa kuutangaza ujumbe wake?

9. Tangazeni katika ikulu za Ashdodi,na katika ikulu za nchi ya Misri:“Kusanyikeni kwenye milimainayoizunguka nchi ya Samaria,mkajionee msukosuko mkubwana dhuluma zinazofanyika humo.”

10. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu hawa wameyajaza majumba yaovitu vya wizi na unyang'anyi.Hawajui kabisa kutenda yaliyo sawa!

11. Kwa hiyo, adui ataizingira nchi yao,atapaharibu mahali pao pa kujihami,na kuziteka nyara ikulu zao.”

Amosi 3