1 Mambo Ya Nyakati 24:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Hayo ndiyo makundi ya wazawa wa Aroni. Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

2. Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, wala hawakuwa na watoto; kwa hiyo ndugu zao Eleazari na Ithamari wakawa makuhani.

3. Mfalme Daudi aliwapanga wazawa wa Aroni katika makundi kufuatana na huduma zao. Alisaidiwa kufanya hivyo na Sadoki, mzawa wa Eleazari, na Ahimeleki, mzawa wa Ithamari.

4. Kwa vile ambavyo kulipatikana viongozi wanaume wengi zaidi miongoni mwa wazawa wa Ithamari, waliwagawanya wazawa wa Eleazari chini ya viongozi kumi na sita, na wazawa wa Ithamari chini ya viongozi wanane.

1 Mambo Ya Nyakati 24