1 Mambo Ya Nyakati 16:35-40 Biblia Habari Njema (BHN)

35. Mwambieni Mwenyezi-Mungu:Utuokoe, ee Mungu wa wokovu wetu,utukusanye pamoja na kutuokoa kutoka kwa mataifa,tupate kulisifu jina lako takatifu,kuona fahari juu ya sifa zako.

36. Asifiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli,tangu milele na hata milele!Kisha watu wote wakasema, “Amina!” Pia wakamsifu Mwenyezi-Mungu.

37. Hivyo, mfalme Daudi akawaacha Asafu na nduguze Walawi mahali walipoliweka sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, kwa ajili ya huduma zinazotakiwa mbele ya sanduku kila siku.

38. Obed-edomu, mwana wa Yeduthuni, pamoja na wenzake sitini na wanane waliwasaidia. Obed-edomu mwana wa Yeduthuni na Hosa walikuwa walinzi wa malango.

39. Mfalme Daudi akawaweka kuhani Sadoki na makuhani wenzake kuwa wahudumu wa hema ya Mwenyezi-Mungu iliyokuwa mahali pa kuabudu huko Gibeoni

40. ili kutolea Mwenyezi-Mungu sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya sadaka za kuteketezwa daima asubuhi na jioni, kulingana na yote yaliyoandikwa katika sheria ya Mwenyezi-Mungu aliyowaamuru Waisraeli.

1 Mambo Ya Nyakati 16