1. Mwombeni Mwenyezi-Mungu awape mvua za masika.Mwenyezi-Mungu ndiye aletaye mawingu ya mvua;ndiye awapaye watu mvua za rasharasha,na kustawisha mimea shambani kwa ajili ya wote.
2. Vinyago vyao vya kupigia ramli ni upuuzi mtupu,na waaguzi wao wanaagua uongo;watabiri wao wanatabiri ndoto za danganyifu,na kuwapa watu faraja tupu.Ndio maana watu wa Yuda wanatangatanga kama kondoo;wanataabika kwa kuwa wamekosa mchungaji.
3. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nimewaka hasira dhidi ya hao wachungaji,nami nitawaadhibu hao viongozi.Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi,nitalitunza kundi langu, ukoo wa Yuda.Nitawafanya kuwa farasi wangu hodari wa vita.
4. Kwa ukoo wa Yuda kutatokea:Watawala wa kila namna,viongozi imara kama jiwe kuu la msingi,walio thabiti kama kigingi cha hema,wenye nguvu kama upinde wa vita.
5. Watu wa Yuda watakuwa kama mashujaa vitaniwatawakanyaga maadui zao katika tope njiani.Watapigana kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nipo pamoja nao;nao watawaaibisha hata wapandafarasi.
6. “Watu wa Yuda nitawaimarisha;nitawaokoa wazawa wa Yosefu.Nitawarejesha makwao kwa maana nawaonea huruma,nao watakuwa kana kwamba sikuwa nimewakataa.Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wao,nami nitayasikiliza maombi yao.