Yoeli 3:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Wakati huo na siku hizonitakapoirekebisha hali ya Yuda na Yerusalemu,

2. nitayakusanya mataifa yote,niyapeleke katika bonde liitwalo,‘Mwenyezi-Mungu Ahukumu.Huko nitayahukumu mataifa hayo,kwa mambo yaliyowatendea watu wangu Israeli,hao walio mali yangu mimi mwenyewe.Maana waliwatawanya miongoni mwa mataifa,waligawa nchi yangu

3. na kugawana watu wangu kwa kura.Waliwauza wavulana ili kulipia malaya,na wasichana ili kulipia divai.

4. “Mnataka kunifanya nini enyi Tiro na Sidoni na maeneo yote ya Filistia? Je, mna kisasi nami mnachotaka kulipiza? Kama mnalipiza kisasi, mimi nitawalipizeni mara moja!

Yoeli 3