13. Enyi makuhani, jivikeni magunia kuomboleza,lieni enyi wahudumu wa madhabahu.Ingieni hekaluni mkaomboleze usiku kucha!Sadaka za nafaka na kinywaji zimetoweka nyumbani kwa Mungu.
14. Toeni amri watu wafunge;itisheni mkutano wa kidini.Kusanyeni wazee na wakazi wote wa nchi,nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu,na humo mkamlilie Mwenyezi-Mungu.
15. Ole wetu kwa ile siku ya Mwenyezi-Mungu,siku hiyo ya Mwenyezi-Mungu inakaribia;inakuja pamoja na maangamizi,kutoka kwa Mungu Mkuu.
16. Mazao yetu yameharibiwa huku tunatazama.Furaha na kicheko vimetoweka nyumbani kwa Mungu wetu.
17. Mbegu zinaoza udongoni;ghala za nafaka ni ukiwa mtupu,ghala zimeharibika,kwa kukosa nafaka ya kuhifadhi.