1. Neno la Mwenyezi-Mungu lililomjia Yoeli, mwana wa Pethueli:
2. Sikilizeni kitu hiki enyi wazee;tegeni sikio wakazi wote wa Yuda!Je, jambo kama hili limewahi kutokea maishani mwenu,au nyakati za wazee wenu?
3. Wasimulieni watoto wenu jambo hili,nao wawasimulie watoto wao,na watoto wao wakisimulie kizazi kifuatacho.
4. Nzige, makundi kwa makundi, wameivamia mimea;kilichoachwa na nzige kimeliwa na tunutu,kilichoachwa na tunutu kimeliwa na parare,kilichoachwa na parare kimeliwa na matumatu.
5. Enyi walevi, levukeni na kulia;pigeni yowe, enyi walevi wa divai;zabibu zote za kutengeneza divai mpya zimeharibiwa.