11. Nimejaa hasira ya Mwenyezi-Mungu dhidi yao.Nashindwa kuizuia ndani yangu.Mwenyezi-Mungu akaniambia:“Imwage hasira barabarani juu ya watotona pia juu ya makundi ya vijana;wote, mume na mke watachukuliwa,kadhalika na wazee na wakongwe.
12. Nyumba zao zitapewa watu wengine,kadhalika na mashamba yao na wake zao;maana nitaunyosha mkono wangu,kuwaadhibu wakazi wa nchi hii.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
13. Wote, tangu mdogo hadi mkubwa kabisa,kila mmoja anatamani kupata faida isiyo halali.Tangu manabii hadi makuhani,kila mmoja wao ni mdanganyifu.
14. Wameliponya jeraha la watu wangu juujuu,wanasema; ‘Amani, amani’,kumbe hakuna amani yoyote!
15. Je, waliona aibu walipofanya machukizo hayo?La! Hawakuona aibu hata kidogo.Hawakujua hata namna ya kuona aibu.Kwa hiyo wataanguka pamoja na wale waangukao;wakati nitakapowaadhibu,wataangamizwa kabisa.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
16. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Simameni katika njia panda, mtazame.Ulizeni mjue juu ya matukio ya zamani.Tafuteni mahali ilipo njia nzurimuifuate nanyi mtapumzisha nafsi zenu.Lakini wao wakasema:‘Hatutafuata njia hiyo.’
17. Kisha nikawawekea walinzi, nikawaambia:‘Sikilizeni ishara ya tarumbeta.’Lakini wao wakasema: ‘Hatutaisikiliza.’
18. “Kwa hiyo, sikilizeni enyi mataifa;enyi jumuiya ya watu jueni yatakayowapata.