1. Kimbieni huko na huko mjini Yerusalemu;pelelezeni na kujionea wenyewe!Chunguzeni masoko yakemwone kama kuna mtu atendaye hakimtu atafutaye ukweli;akiwako, basi Mwenyezi-Mungu atausamehe Yerusalemu.
2. Ingawa wanaapa: “Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo”,viapo vyao ni vya uongo.
3. Ee Mwenyezi-Mungu, wewe watafuta daima uaminifu.Umewatwanga, lakini hawakuona uchungu;umewateketeza, lakini walikataa kukosolewa.Wamezifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba;wamekataa kabisa kurudi kwako.
4. Ndipo nilipowaza:“Hawa ni watu duni hawana akili;hawajui matakwa ya Mwenyezi-Mungu,hawajui Sheria ya Mungu wao.
5. Nitawaendea wakuu niongee nao;bila shaka, wao wanajua matakwa ya Mwenyezi-Mungu;wanajua sheria ya Mungu wao.”Lakini wote waliivunja nira yao.Waliikatilia mbali minyororo yao.
6. Kwa hiyo simba kutoka msituni atawaua;mbwamwitu kutoka jangwani atawararua.Chui anaivizia miji yao.Kila atokaye humo atararuliwa vipandevipande,kwa sababu dhambi zao ni nyingi,maasi yao ni makubwa.
7. Mwenyezi-Mungu anauliza:“Nitawezaje kukusamehe ee Yerusalemu?Watu wako wameniasi;wameapa kwa miungu ya uongo.Nilipowashibisha kwa chakula,wao walifanya uzinzi,wakajumuika majumbani mwa makahaba.
8. Walikuwa kama farasi walioshiba wenye tamaa,kila mmoja akimtamani mke wa jirani yake.
9. Je, nisiwaadhibu kwa mambo haya yote?Nisilipize kisasi juu ya taifa kama hili?