Yeremia 48:1-14 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi:“Ole watu wa Nebo, maana mji wake umeharibiwa!Kiriathaimu umeaibishwa, umetekwa,ngome yake imebomolewa mbali;

2. fahari ya Moabu imetoweka.Mpango ulifanywa huko Heshboni dhidi yake:‘Haya! Tuwaangamize wasiwe tena taifa!’Nawe Madmeni utanyamazishwa,upanga utakufuatia.

3. Sikiliza! Kilio kutoka Horonaimu:‘Maangamizi na uharibifu mkubwa!’

4. Moabu tayari imeangamizwakilio chake chasikika mpaka Soari.

5. Walionusurika wanapanda kwenda Luhithihuku wanalia kwa sauti.Wanapoteremka kwenda Horonaimu,wanasikia kilio cha uharibifu.

6. Kimbieni! Jiokoeni wenyewe!Kimbieni kama pundamwitu jangwani!

7. “Moabu, ulitumainia ngome na hazina zako,lakini sasa wewe pia utatekwa;mungu wako Kemoshi atapelekwa uhamishonipamoja na makuhani na watumishi wake.

8. Mwangamizi atapita katika kila mji,hakuna mji utakaomwepa;kila kitu mabondeni kitaangamianyanda za juu zitaharibiwa,kama alivyosema Mwenyezi-Mungu.

9. Mchimbieni Moabu kaburi,maana kuangamia kwake ni hakika;miji yake itakuwa tupu,bila mkazi hata mmoja.

10. Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Mwenyezi-Mungu kwa ulegevu; alaaniwe anayezuia upanga wake usimwage damu!

11. Moabu amestarehe tangu ujana wake,ametulia kama divai katika gudulia.Hajamiminiwa toka chombo hata chombo,hajapata kuchukuliwa uhamishoni.Kwa hiyo yungali na ladha yake,harufu yake nzuri haijabadilika kamwe.

12. “Kwa hiyo, wakati waja, nasema mimi Mwenyezi-Mungu ambapo nitampelekea wamiminaji ambao wataimimina divai yake. Wataimwaga yote kutoka vyombo vyake na kuvivunja vipandevipande.

13. Hapo Wamoabu watamwonea aibu mungu wao Kemoshi, kama vile watu wa Israeli walivyomwonea aibu Betheli, mungu waliyemtegemea.

14. Mwawezaje kusema: ‘Sisi ni mashujaa,na watu wenye nguvu nyingi za vita?’

Yeremia 48