Yeremia 23:17-29 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Wao hawakomi kuwaambia wale wanaodharau neno langu mimi Mwenyezi-Mungu: ‘Mambo yatawaendea vema.’ Na kumwambia kila mtu afuataye kwa ukaidi fikira zake; ‘Hakuna baya lolote litakalokupata!’”

18. Lakini, ni yupi kati ya manabii haoaliyepata kuhudhuria baraza la Mwenyezi-Mungu,hata akasikia na kuelewa neno lake?Au ni nani aliyejali neno lake,hata akapata kulitangaza?

19. Tazama, dhoruba kutoka kwa Mwenyezi-Mungu!Ghadhabu imezuka;kimbunga cha tufanikitamlipukia mtu mwovu kichwani.

20. Hasira ya Mwenyezi-Mungu haitarudi nyuma,mpaka atakapotekeleza na kukamilishamatakwa ya moyo wake.Siku zijazo mtayaelewa vema mambo hayo.

21. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Mimi sikuwatuma hao manabii,lakini wao walikwenda mbio;sikuwaambia kitu chochote,lakini wao walitabiri!

22. Kama wangalihudhuria baraza langu,wangaliwatangazia watu wangu maneno yangu,wakawageuza kutoka katika njia zao mbovu,na kutoka katika matendo yao maovu.

23. “Mimi ni Mungu aliye karibu, si Mungu aliye mbali.

24. Je, mtu aweza kujificha mahali pa siri hata nisiweze kumwona? Hamjui kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nipo kila mahali, mbinguni na duniani? Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

25. Mimi nimeyasikia maneno waliyosema hao manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema, ‘Nimeota ndoto, nimeota ndoto!’

26. Itakuwa hivyo mpaka lini? Hao manabii wataendelea mpaka lini kupotoka moyo; kutabiri uongo na udanganyifu wa mioyo yao wenyewe?

27. Kwa ndoto zao hizo wanapanga kuwafanya watu wangu wanisahau mimi kama baba zao walivyonisahau, wakamwendea Baali!

28. Nabii aliyeota ndoto, na aitangaze ndoto yake, lakini yeye aliye na neno langu, na alitangaze kwa uaminifu. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema, makapi si sawa na ngano!

29. Neno langu ni kama moto; ni kama nyundo ipasuayo miamba vipandevipande.

Yeremia 23