13. Tazama, mimi sasa napambana nanyi mnaoishi bondeni,mnaokaa kwenye mwamba wa tambarare,nyinyi mnaosema, ‘Nani atathubutu kutushambulia?Nani awezaye kuingia katika makazi yetu?’
14. Nitawaadhibu kadiri ya matendo yenu;mimi Mwenyezi-Mungu nasema.Nitawasha moto katika msitu wenunao utateketeza kila kitu kinachouzunguka.”