Yeremia 2:11-17 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Kwamba kuna taifa lililowahi kubadilisha miungu yakeingawa miungu hiyo si miungu!Lakini watu wangu wameniacha mimi, utukufu wao,wakafuata miungu isiyofaa kitu.

12. Shangaeni enyi mbingu, juu ya jambo hili,mkastaajabu na kufadhaika kabisa.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

13. Maana, watu wangu wametenda maovu mawili;wameniacha mimi niliye chemchemi ya maji ya uhai,wakajichimbia visima vyao wenyewe,visima vyenye nyufa, visivyoweza kuhifadhi maji.

14. “Je, Israeli ni mtumwa,ama amezaliwa utumwani?Mbona basi amekuwa kama mawindo?

15. Simba wanamngurumia,wananguruma kwa sauti kubwa.Nchi yake wameifanya jangwa,miji yake imekuwa magofu, haina watu.

16. Isitoshe, watu wa Memfisi na Tahpanesi,wameuvunja utosi wake.

17. Israeli, je, hayo yote si umejiletea mwenyewe,kwa kuniacha mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako,niliyekuwa ninakuongoza njiani?

Yeremia 2