7. Tazama! Ni machela ya Solomoni;amebebwa juu ya kiti chake cha enzi;amezungukwa na walinzi sitini,mashujaa bora wa Israeli.
8. Kila mmoja wao ameshika upanga,kila mmoja wao ni hodari wa vita.Kila mmoja ana upanga wake mkononi,tayari kumkabili adui usiku.
9. Mfalme Solomoni alijitengenezea machela,kwa mbao nzuri kutoka Lebanoni.